USISAHAU KUMUOMBEA DUA YULE ALIYEKUPA FAIDA YA KIELIMU .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa:  https://www.fawaidusalafiyatz.net

USISAHAU KUMUOMBEA DUA YULE ALIYEKUPA FAIDA YA KIELIMU

قال أبو محمد -رزق الله- التميمي الحنبلي- رحمه الله- :

Amesema Abuu Muhammad Rizqullah Tamiimiy Al-hanbaliy -Allah amrahamu-:

يقبح بكم أن تستفيدوا منا ثم تذكرونا ولا تترحموا علينا.

Inakuwa ni vibaya kwenu mukafaidika na sisi kisha (mukawa) munatutaja na wala hamuturehemu.

المصدر : الإلماع/للقاضي عياض

Maelezo ya mfasiri:

Ndugu yangu tambua kuwa yule aliyekupa faida ya kielimu inawajibika umfanyie yafuatayo :

1- Uiegemeze elimu kwake .

2- Umrehemu/umuombee dua pindi anapotajwa.

Na bila shaka katika sababu za kubarikiwa katika elimu ni kuiegemeza faida kwa yule uliyeisikia kutoka kwake kama wanavyosema wanavyuoni :

مَنْ بَرَكة الْعِلْمِ عَزْوُ كُلِّ قَوْلٍ إِلى قَائِلِهِ

Miongoni mwa baraka ya elimu ni kuigemeza kila kauli kwa mzungumzaji wake.

وقال الإمام ابن عبد البرّ المالكي – رحمه الله – المتوفى سنة ٤٣٦ه‍ :

Amesema imamu ibn ‘Abdil-Barr Al-Maalikiy- Allaha amrahamu- aliyefariki mwaka 436 baada ya hijra:

يُقال : إن من بركة العلم أن تضيف الشئ إلى قائله .

Kunasemwa: Bila shaka katika baraka ya elimu ni kukiegemeza kitu kwa msemaji wake .

المصدر: جامع بيان العلم وفضله “٨٩/٢”

Pia katika haki ya mwanafunzi kwa mwalimu wake kwa maana kwa yule aliyefaidika naye kielimu ni kumuombea dua na huu ni uchache kabisa ambao  utamlipa mwalimu kama alivyosema sheikh Abdu Ssalam Asshuwair- Allah amuhifadhi- na akasema pia katika njia za wanachuoni pindi wanapoandika vitabu vyao  hujiombea dua wenyewe na wazazi wao na mashekhe zao.

Tanbih:

Inaingia vilevile katika nyanja za kufanya tarjama makala mbalimbali kama umenufaika kutoka katika kazi ya mwenzako kwa kunukuu faida fulani basi iegemeze kwake kufanya kwako hivyo ni sababu ya kubarikiwa katika elimu yako , na wale wanao copy na kupest makala za watu wengine bila shaka hawa pamoja na kufanya kwao khiyana bila shaka wana sehemu kubwa ya kutopata baraka katika elimu zao .

Mwisho:Namuomba Allah aturehemu sisi na wazazi wetu na mashekhe zetu wote.

Mfasiri : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 6, 1443H ≈ Jan 9, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

        •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *