USIWE KATIKA JESHI LA IBILISI!

◾️ قال ابن القيم- رحمه الله-:

Amesema ibn l-Qayyim – Allah amrahamu – :

▫️ الحاسدَ تُعِينُهُ الشياطينُ بلا استدعاء منه للشيطان؛

Hasidi husaidiwa na Mashetani bila ya yeye kuwaita (hao) Mashetani,

لأن الحاسد شبيهٌ بإبليس وهو في الحقيقة من أتباعه؛

Kwa sababu hasidi anafanana na Ibilisi, naye kwa hakika ni katika wafuasi wake huyo (Ibilisi) ;

  • لأنه يطلبُ ما يحبه الشيطان من فساد الناس وزوال نعم الله عنهم،

Kwa sababu huyo (hasidi) hutafuta kile anachokitaka Shetani kama vile kuharibikiwa watu na kuondokewa na neema za Allah

كما أن إبليس حسد آدم لشَرَفَه وفضله،

Kama vile Ibilisi alivyomhusudu Adamu kwa sababu ya utukufu wake na ubora wake,

وأبى أن يسجدَ له حَسَدًا، فالحاسد من جند إبليس.

Na akakataa kumsujudia kwa hasadi(tu) , basi hasidi ni katika jeshi la Ibilisi.

[ بدائع الفوائد].

Maelezo ya mfasiri :

Hasidi ni katika wafuasi wa Ibilisi na kile anachokifanya cha kuwahusudu watu husaidiwa na Mashetani, na hasidi humuita shetani ili amsaidie katika uovu wake huo bila yeye mwenyewe huyo hasidi kujijua, kwa ajili hii basi hasidi ni mfuasi wa Ibilisi,kwa sababu tabia yake ni kama tabia ya Ibilisi ya kupenda watu waharibikiwe na kuondokewa na neema za Allah!, kama ilivyokuwa kwa huyo Ibilisi yeye alimhusudu Adamu – amani iwe juu yake – kwa sababu ya utukufu wake huyo Adamu na ubora aliopewa na Allah na akakataa kumsujudia Adamu sijida ya heshima na sababu ya kukataa ni husuda aliyokuwa nayo kwa Adam kwa hiyo hasidi ni katika jeshi la Ibilisi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo nane  11, 1445H ≈ Nov  25, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

       •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *