MANENO MAZITO ALIYOYAANDIKA SHEIKH SWALEH AL-‘USWAIM- ALLAH AMUHIFADHI -KATIKA UKURASA WAKE WA TWITTER TAREHE 26 MFUNGO TISA ,1443H – JAN,29,2022M :
في الخلق من يبغض أحدًا بهواه، وتزين له نفسه أنَّ فعله دين الله، ويُسارع في كل مناسبةٍ لينال منه،
Katika viumbe kuna yule anayemchukia (mtu) fulani kwa matamanio yake (mabaya) ,na nafsi yake inampambia kuwa anachokifanya ni dini ya Allah na anaenda mbio katika kila munasaba ili amchafue huyo (mtu),
ويجتهد ليصرف النَّاس عنه، ويمنع انتفاعهم به؛
Na anajitahidi ili awaepushe watu(na mtu) huyo na anawazuia (watu) na kunufaika naye
فينوب في الشَّرِّ عن إبليس، ويُحاذيه في زخرفة التَّلبيس،
Basi (mtu huyu) anakuwa naibu wa Ibilis katika (kufanya) shari, na anafanana naye katika kuyapamba (maneno ya) kuwafachanganya (watu) ,
فعليه وزر النِّيابة وإثم الغَواية.
Basi (mwenye tabia hii) ana madhambi ya kufanya kazi ya Ibilis, na madhambi ya kuwapoteza watu .
Maelezo ya mfasiri:
Hawa watu wamejaa mno -Allah asiwakithirishe mfano wao- ,watu ambao huwachukia watu kwa matamanio yao bila ya mizani ya kisheria ima anaweza akamchukia mtu kwa kuwa hakifuati kile anachokitaka yeye ambacho hakipo katika sheria, tena mbaya zaidi nafsi yake inampambia kuwa hiki anachokifanya ni dini na njia ya sawa na huwa anajitajidi katika kila kikao au munasaba fulani kumtukana au kumponda au kumchafua kwa watu huyo anayemchukia, na hufanya juhudi zake zote ili watu wamkimbie na wasinufaike naye kisha sheikh -Allah amuhifadhi- akaeleza kuwa mtu mwenye tabia hii huyu anafanya kazi anayoifanya Ibilisi kwa maana ni naibu wake katika kuwazuia watu na heri na vile vile anafanana na Ibilisi katika kuyapamba maneno yake ili kuupamba ule upotevu wake basi mtu mwenye tabia hii ana madhambi mara mbili :
1- Madhambi ya kufanya kazi ya Ibilisi na kuwa naibu wake kwa kuwazuia watu na heri.
2- Madhambi ya kuwapoteza watu.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo tisa 28, 1443H ≈ Jan 31, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•