Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
افْتِرَاءَاتُ الرَّافِضِيِّ عَلِيّ جُمْعَة
مَيُوْنغ التَّنْزَانِيِّ عَلَى الْخَلِيْفةِ الرَّاشِدِ عُمَرَ بْنِ الخِطَّاب- رضي الله عنه-
UZUSHI WA MSHIA ALIYY JUMA MAYUNGA JUU KHALIFA MUONGOFU UMAR BIN L-KHATTWAAB-ALLAH AMRIDHIE-
قَالَ هَذا الضَّالُّ الَّذِي شَابَتْ لِحْيَتُهُ وَ رَأْسُهُ وانْهَدَّتْ قُوَاه وَهُوَ عَلى بَاطِلِهِ – :
AMESEMA HUYU MPOTEVU AMBAYE NDEVU ZAKE ZIMEOTA MVI NA KICHWA CHAKE, NA NGUVU ZAKE ZIMEDHOOFIKA HALI YA KUWA YUPO JUU YA UPOTEVU WAKE :-
” Umar bin Khattab amezua swala ya Tarawih.Yeye ni mtu wa kwanza kuharamisha ndoa ya Mut’a.Umar ndiye aliyezua takbira nne katika swala ya Jeneza ” .
📝QUR’AN INAYOBAINISHA.
Tarjama na Tafsiri
Kiarabu na Kiswahili , ukurasa: 1437,katika maelezo ya aya 44 ya suuratul haaqqah.
MAELEZO YA MWANDISHI:
Maneno haya ameyanasibisha katika Tarekh l-kholafai cha Suyuutiy , lakini cha kuustajabisha haya ambayo Mayunga amedai kuwa ni katika mambo ambayo ameyazusha Umar -Allah amridhie- haya yote yamethibiti kutoka kwa Mtume (swala na salamu za Allah zimfikie)
mfano: Swala na tarawehe iliswaliwa na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- lakini aliacha kwa kuhofia kuwa huenda ikafaradhishwa kwa ummah lakini hakuikataza kwa hiyo Omar alichofanya ni kuhuisha suna tu.
Ama ndoa ya Mut’a haikuharamishwa na Omar bali aliiharamisha Mtume (swala na salamu za Allah zimfikie)
Ama takbira nne za jeneza hakuna dalili inayo onesha kuwa zilianzishwa na Omar bali hili ni maarufu kuwa takbira nne za jeneza ni sunna .
Nimeacha kutaja na kunukuu hadithi zinazo julisha kuwa haya yalifanywa na Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- kwa sababu haya ni maarufu kwa waislamu haina haja ya kunukuu hadithi na makala ikawa ndefu, ili nilitaka kuwabainishia waislamu chuki za mashia kwa maswahaba wa Mtume na haswa Watanzania ambao baadhi yao hudanganywa kuwa Mashia wa Tanzania hawawatukani Maswahaba.
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal ,1, 1442H ≈ May 19, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•