VIGAWANYO VYA KUKUSUDIA UOVU NA HUKUMU ZAKE.

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

Makala namba (1) .

✍ قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله:

Amesema shekh ibn Uthaimin -Allah amrehemu-:

▪️فإن هم بالسيئة ولم يعملها، فالأدلة تدل على أن ذلك أقسام:

Basi kama (mtu) atakusudia (kufanya) uovu na akawa hajaufanya, dalili zinajulisha kuwa hilo lina vigawanyo (kadhaa):

⬅️ القسم الأول:

Kigawanyo cha kwanza:

أن يتركها عجزا عنها، مع فعل ما قدر عليه منها، فهذا يكتب عليه إثما كاملا، كإثم فاعلها،

(Ni Mtu) kuuacha huo (uovu) kwa kushindwa pamoja na kufanya yale aliyoyaweza katika kuufikia huo (uovu) , basi mtu huyu huandikiwa dhambi iliyokamilika kama vile dhambi ya aliyeufanya huo (uovu) .

ودليله قول النبي صلى الله عليه وسلم:

“إذا التقى المسلمين بسيفهما، فالقاتل والمقتول في النار “، قالوا هذا القاتل ، فما بال المقتول؟ قال :”لأنه كان حريصا على قتل صاحبه “.

Na dalili yake ni kauli ya Mtume swala na salamu za Allah ziwe juu yake:

“Pindi watakapopambana waislam wawili kwa mapanga yao basi muuaji na muuliwa (wote) motoni”

wakasema (Maswahaba) huyu ni muuaji ,basi ni lipi kosa la alilolifanya muuliwa ? akasema :

” Ni kwa sababu yeye alikua ni mwenye pupa ya kumuua mwenzake”.

📚 التعليق على مسلم (مج ١ ص ٣٨٠ – ٣٨١).

Maelezo ya mpitiaji:

Kigawanyo cha kwanza ni yule anayepata madhambi sawa na mfanyaji naye ni huyu aliyemtaja sheikh hapa kwa maana ni yule aliyekusudia uovu na akaendelea na maazimio yake na akafanya sababu zote za kuuendea huo uovu, na kukawa hakuna kilichomzuia na kufanya huo uovu isipokuwa ni kizuizi kilichoshindikana basi mtu huyu anaandikiwa dhambi mfano wa dhambi ya yule aliyefanya :

Mfano wa hili ni hii hadithi aliyoitaja hapo sheikh -Allah amrahamu- hawa waislamu wawili wanaopambana na kila mmoja anakusudia na kuazimia kumuua mwenzie na kila mmoja amefanya sababu ya kulitekeleza hilo , ndiyo maana hata huyu aliyeuliwa naye ana pata madhambi sawa na yule aliyemuua .

Mfano mwingine: Mwanamume aliyekaa sehemu fulani kisha akasikia sauti za wanawake ,akakusudia na kuazimia kugeuka nyuma ili azione sura zao lakini alipogeuka akaona kizuizi cha ukuta baina yake na hao wanawake kwa hiyo hakufanikiwa kuwaona , lakini maadamu aliazimia maazimio ya moja kwa moja na hakuna kilichomzuia isipokuwa ukuta basi anaandikiwa madhambi ya kuwatezama hao wanawake .

Kwa hiyo kila aliyekusudia kufanya madhambi na akaazimia maazimio ya moja kwa moja na akaendelea na maazimio hayo na akafanya sababu za kufanya dhambi hiyo , lakini kikatokea kizuizi kilichomzuia kufanya hayo madhambi pamoja na maazimio yaliyopo katika moyo wake basi mtu huyu anaandikiwa dhambi kamili kwa sababu ya makusudio yake .

Na kanuni ya kifiqih inasema:

الْأُمُوْرُ بِمَقَاصِدِهَا .

Mambo (hali, vitendo,) huhukumiwa kwa makusudio yake.

Imepitiwa na : Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 6, 1443H ≈ October 12, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *