Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
VIGAWANYO VYA KUKUSUDIA UOVU NA HUKUMU ZAKE .
Makala namba ( 3):
✍ قال الشيخ ابن عثيمين -رحمه الله-:
Amesema shekh ibn Uthaimin -Allah amrehemu- :
⬅️ القسم الثالث :
Kigawanyo cha tatu:
أن يهم بالسيئة، ثم يتركها لله تعالى، فهذا تكتب له حسنة كاملة ،
(Ni mtu) kukusudia uovu kisha akauacha kwa ajili ya Allah aliyetukuka, basi (mtu) huyu huandikiwa jema moja lililokamilika ,
لقوله تبارك وتعالى في الحديث القدسي:
“{فإنما تركها من جراىٔي”}
kwa kauli ya Allah- aliyetukuka- katika hadithi takatifu:
“Basi hakika si vinginevyo ameuacha huo (uovu) kwa ajili yangu” .
📚 التعليق على مسلم (مج ١ ص ٣٨٠ – ٣٨١).
Maelezo ya mpitiaji:
Mwenye kukusudia shari na akaazimia na akawa na pupa ya kuufanya huo uovu lakini akaacha kuufanya huo uovu kwa kumwogopa Allah mtu huyu anaandikiwa jema moja .
Mfano: Mwanamume amekubaliana kukutana na mwanamke ili wakazini ,na akaazimia kufanya hivyo na akapupia lakini pindi alipokuwa anaenda kukutana naye njiani akaiambia nafsi yake kuwa: Allah amekataza uzinifu ,iweje mimi nimuasi Allah kwa uchafu huu ,akarudi na akaacha kuzini kwa hofu ya kumuogopa Allah ,basi mtu huyu anaandikiwa jema moja .
Au mtu alikusudia kwenda kuiba dukani na alipofika dukani akalikuta lipo wazi na alipotaka kuchukua ikamjia hofu ya kumuogopa Allah katika moyo wake na akaacha kuiba huyu naye anaandikiwa jema moja ,n.k
Mpitiaji: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 11, 1443H ≈ October 17, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•