VIGAWANYO VYA KUKUSUDIA UOVU NA HUKUMU ZAKE. (Makala namba) 2 .

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

VIGAWANYO VYA KUKUSUDIA UOVU NA HUKUMU ZAKE .

Makala namba: ( 2)

✍ قال الشيخ ابن عثيمين رحمه الله:

Amesema shekh ibn Uthaimin- Allah amrehemu-:

⬅️ القسم الثاني

Kigawanyo cha pili:

أن يتركها عجزا، دون أن يفعل الأسباب، ودون أن يفعل ما قدر عليه منها ،

Ni mtu kuacha kufanya (ovu) kwa kushindwa, na bila kufanya sababu ,na bila kufanya zile anazoziweza katika hizo (sababu za kuuendea),

كرجل همّ بسرقة، ولكنه رأى الناس حوله ، فتركها،

kama vile mtu alikusudia kuiba lakini akawaona watu pembezoni mwake akaacha (kuiba)

فهذا عليه وزرها، لكنه ليس كالذي فعل ما قدر عليه منها ،

basi (mtu) huyu ana madhambi lakini si kama yule ambaye amefanya yale aliyoyaweza katika hizo (sababu za kuiba)

لأن هذا لم يفعل شيئا، لكن عليه الوزر، وهو وزر النية بلا شك .

Kwa sababu huyu hakufanya chochote, lakini anapata dhambi, nayo ni dhambi ya nia (tu) bila shaka.

📚 التعليق على مسلم
(مج ١ ص ٣٨٠ – ٣٨١).

Maelezo ya mpitiaji:

Kigawanyo cha pili : ni mtu aliyekusudia kufanya uovu lakini hakuufanya huo uovu na hakufanya juhudi na sabababu za kuufanya huo uovu mfano wake ni huyu aliyemtaja sheikh hapa :

Mtu aliyekusudia kuiba sehemu fulani lakini alipopita akaona kuna watu wapo maeneo haya alipoona hivyo akaacha kuiba ,bila shaka huyu anapata madhambi ya nia na kukusudia kwake kuiba ,lakini makosa yake hayalingani na yule aliyekusudia na akafanya juhudi na sababu za kuufanya uovu huo kama vile yule aliyekusudia kuiba na akavunja mlango wa nyumba lakini akakutana na mlango mwingine mgumu akashindwa na akaacha kuiba basi bila shaka huyu anaandikiwa dhambi ya wizi iliyokamilika .

Mpitiaji: Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 8, 1442H ≈ October 14, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *