Vikadi vya akidah kwa watoto wa kiislam

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

KITABU CHA PILI :

17 – Mtiririko /Mfululizo wa makala za vikadi vya aqida /itikadi kwa watoto wa kiislamu .

س رقم: ١٧

Swali no.17 :

مَا هِيَ أَرْكَانُ الْإِيْمَانِ ؟

Ni zipi nguzo za imani ?

ج:
Jawabu:

أَرْكَانُ الْإِيْمَانِ سِتَّةٌ:

Nguzo za imani ni sita (nazo ni) :

الْإِيْمَانُ بِاللّٰهِ، وَمَلَائِكَتِهِ، وَكُتُبِهِ،وَرُسُلِهِ،وَالْيَوْمِ الْآخِرِ ،وَبِالْقَدَرِ خَيْرِهِ وَشَرِّهِ.

Kumuamini Allah,na Malaika wake,na vitabu vyake,na Mitume yake,na siku ya mwisho,na (kuamini) kadari ya heri yake na shari yake.

سلسلة بطاقات: العقيدة لأشبال الإسلام, المؤلف: د. أحمد بن مبارك بن قذلان المزروعي.

[ Mtiririko wa makala za vikadi vya aqidah/itikadi kwa watoto wa kiislamu, Mtunzi: D. Ahmad bin Mubaarak bin Qadh-laan Al-maz-ruuiy Allah amuhifadhi]

Maelezo ya mfasiri:

Mzazi/mlezi hapa atamuelezea mtoto kwa kumwambia :

Mwanangu tambua kuwa imani yako haiwezi kukamilika mpaka uamini hizi nguzo sita za imani, na kiwango cha chini kabisa cha imani ambacho mtu akiamini hicho anakuwa muislamu ni Kama ifuatavyo:

Nguzo ya kwanza, kumuamini Allah, nguzo hii imekusanya mambo manne:

1- Kuamini kuwepo kwa Allah.

2- kumpwekesha katika matendo yake .

3-Kumpwekesha katika ibada

4-Kumpwekesha katika majina yake na sifa zake .

Nguzo ya pili,kuamini Malaika ambayo imekusanya mambo mawili:

1- Kuamini kuwa hao Malaika ni viumbe wa Allah -aliyetukuka-.

2- Na katika hao Malaika kuna yule anayeteremka na wahyi kwa Mitume.

3- Nguzo ya tatu, kuamini vitabu vya Allah :

Maana yake ni kuamini kuwa Allah ameteremsha vitabu kwa anayemtaka katika mitume yake, na hivyo vitabu ni maneno ya Allah -aliyetukuka-, na lengo la kuviteremsha vitabu ni kuwa watu wahukumiwe na hivyo vitabu ,na vitabu vyote vimefutwa na Quran kwa maana hukumu zinazofanyiwa kazi ni zile zilizokuja katika Qurani tu .

4-Nguzo ya nne ,ni kuamini Mitume :

Kuamini kuwa Allah amewapelekea watu mitume wanaotokana na wao ili wawaamrishe kumuabudia Allah pekee .
Na kuamini kuwa wa mwisho wao ni Muhammad -swala na salamu za Allah zimfikie-.

5-Nguzo ya tano ni kuamini siku ya mwisho:

Maana yake ni kuamini kuwa kuna siku ya kufufuliwa ambayo ni siku ya kiama ,watu watafufuliwa ili walipwe ,na wema wataingizwa peponi na waovu watapewa walichokitenda na malipo yao ni motoni .

6-Nguzo ya sita ni kuamini aliyoyakadiria Allah .

Maana yake ni kuamini kuwa Allah amekadiria kila kitu cha heri au shari tokea mwanzo ambao hauna mwanzo ,na hakuna chochote kinachotokea isipokuwa hutokea kwa matashi yake na yeye ndiye aliyekiumba .

Usikose makala namba 18 inayofuata in shaa Allah

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi (Rajabu) 13, 1444H ≈ Feb 4, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *