VIWILI HIVI HAVIKUSANYIKI PAMOJA !

قال الإمام القرطبي رحمه الله:

Amesema imam Al-Qurtubiyy- Allah amrahamu-:

” وإذا رأيت متكبراً فاعلم أنه قليل الصلاة أو عديمها ؛ لا يجتمع كبر مع كثرة سجود”.

Na utapomuona (mtu) mwenye kiburi basi tambua kuwa huyo ni mchache wa swala au haipo kabisa (kwake hiyo swala) , kiburi hakikusanyiki na wingi wa kusujudu (kuswali) .

[الجامع لأحكام القرآن ٦٩/١

Maelezo ya mfasiri:

Kiburi ni tabia mbaya ambayo imeharamishwa na kiburi maana yake ameieleza Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- pale aliposema :

” الكِبْرُ بَطَرُ الحَقِّ، وغَمْطُ النَّاسِ“

“ Kiburi ni kuikataa haki na kuwadharau watu ” .

Hapa tunajifunza kuwa kukithirisha kuswali na kudumu na swala ni katika mambo yanayoondoa tabia ya kiburi, kwa sababu kitendo cha kuliweka paji lako la uso chini ya ardhi ni kudhihirisha kuwa wewe si chochote si lolote bali ni kiumbe dhalili mbele ya Allah -aliyetukuka- ambaye umemsujudia ,na ukijijua kuwa wewe ni kiumbe dhalili basi utajiepusha na tabia ya kiburi kama alivyosema Al-ahnaf bin Qais -Allah amrahamu-:

عجبًا لابن آدم يتكبر وقد خرج من مجرى البول مرتي

Ni ajabu kwa mwanadamu analeta kiburi na hali yeye bila shaka ametoka kupitia njia ya mkojo mara mbili .

البيهقي في الشعب ،وغيره

Maana ya maneno haya:

Inastaajabisha sana ni vipi binadamu anakuwa na kiburi na hali yeye amezaliwa kupitia njia mbili za mkojo :

1- Njia ya kwanza ni pale alipotolewa hali ya kuwa ni manii kupitia njia ya utupu wa baba yake.

2- Njia ya pili ni pale alipotoka tumboni mwa mama yake kupitia njia ya utupu wa huyo mama yake.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo kumi 20, 1445H ≈ Feb /1, 2023M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *