Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiya.net
VIZUIZI VYA KUMTAMBUA ALLAH ,KUMPENDA ..
🔺 قال ابن القيم رحمه الله:
▪️وسمعت -شيخ الاسلام ابن تيمية – يقول :
في قول النبي “لا تدخل الملائكة بيتا فيه كلب ولا صورة “
Amesema ibn l-Qayyim-Allah amrahamu- : Na nilimsikia sheikh l-islam ibn Taimiyyah akisema:
katika (kufafanua) kauli ya Mtume- “Malaika hawaingii nyumba (ambayo) ndani yake kuna mbwa wala sanamu/picha ” .
إذا كانت الملائكة المخلوقون يمنعها الكلب والصورة عن دخول البيت.
فكيف تلج :
معرفة الله عز وجل
(akasema ibn Taimiyyah):
Ikiwa Malaika (ambao ni) viumbe wanazuiliwa na mbwa na masanamu/mapicha kuingia (ndani) ya nyumba ,basi ni vipi kutaingia utambuzi wa kumjua Allah -aliyeshinda na kutukuka-
ومحبته
وحلاوة ذكره
na mapenzi yake na utamu wa kumtaja huyo (Allah)
والأنس بقربه
في قلب ممتلئ بكلاب الشهوات وصورها؟!!
na kuliwazika kwa kuwa karibu naye , (vipi vitu hivi vitaingia) katika moyo uliojaa mbwa wa matamanio na masanamu /mapicha ya hayo ( matamanio) ?!!
📚 مدارج السالكين .٣٩١/٢
Maelezo:
Ufupi wa maana ya maneno haya ya ibn Taimiyyah-Allah amrahamu- yanayostahiki kuandikwa kwa wino wa dhahabu ni hii :
ikiwa Mtume- swala na salamu za Allah zimfikie- amesema kuwa “Malaika hawaingia nyumba yenye mbwa ndani yake au sanamu /picha” ,na hawa Malaika ni viumbe katika viumbe wa Allah , ikiwa hali ni hiyo ! basi je mtu mwenye moyo mchafu wenye matamanio machafu na maovu kama uzinifu ,liwati,ulevi ,hasadi,mafundo ,n.k ,je moyo huu ndani yake kunaweza kuingia elimu ya kumjua Allah na kutambua haki zake na kuzitekeleza ? ,moyo huu unaweza ukampenda Allah ? moyo huu unaweza ukapata raha kwa kumtaja Allah ? moyo huu unaweza ukapata maliwazo kwa kujikurubisha kwake kwa Allah ? ,bila shaka moyo huu hauwezi ukasifika na sifa hizi.
Tumejifunza kuwa moyo mchafu ni kizuizi cha kumtambua Allah -aliyetukuka- na kumuabudu haki ya kumuabudu ,na ni kizuizi cha kumpenda Allah ,na ni kizuizi cha kupata raha na utulivu wakati wa kumtaja Allah, na ni kizuizi cha kupata maliwazo kwa kujikurubisha kwa Allah !, ujumla wa yote moyo mchafu ni kizuizi cha cha kufanya mema .
Muandaaji: fawaidusalafiya.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiya.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shawwal 22, 1442H ≈ Jun 3, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•