VIZUIZI VYA KUPITA KATIKA NJIA ILIYONYOOKA

قال الشيخ عبدالرزاق_البدر حفظه الله:

Amesema sheikh Abdul-Rrazzaq Al-Badr – Allah amuhifadhi -:

عوائق السير على الصراط المستقيم:

Vizuizi vya kupita juu ya njia iliyonyooka :

ينبغي أن تعلم أيها السائر على هذا الصراط، أن أمامك عوائق تعوق سيرك على هذا الصراط وتقطعك على المضي فيه،

Inatakikana ujue ewe mwenye kupita juu ya njia hii iliyonyooka kuwa mbele yako kuna vizuizi vinavyokuzuia kupita juu ya hii njia iliyonyooka na zinakuzuia kuendelea na (kupita) katika (njia) hiyo,

وهي تحديدا ثلاثة عوائق،

Na hivyo vizuizi kwa kuvibainisha ni vitatu,

جاء في سورة الفاتحة نفسها هدايات عظيمة ودلالات مباركة لتحصيل السبيل الآمنة للنجاة منها،

Kumekuja katika suratul-fatihah yenyewe miongozo mikubwa na dalili zenye baraka za kupata njia yenye amani ili kuokoka kutokana na hivyo (vizuizi)

وهي عوائق نبه عليها أهل العلم كثيرا وحذروا الناس من الوقوع فيها.

Na hivyo vizuizi wamevitanabahisha wanavyuoni mara nyingi, na wakawatahadharisha watu kutokana na kuingia katika hivyo (vizuizi) .

وهي على مراتبها في الخطورة:

Na hivyo (vizuizi) kwa daraja zake katika uhatari ni (kama ifuatavyo) :

العائق الأول: عائق الشرك بالله تعالى.

Kizuizi cha kwanza : Ni kizuizi cha kumshirikisha Allah.

العائق الثاني: عائق البدعة.

Kizuizi cha pili: Ni kizuizi cha uzushi.

العائق الثالث: عائق المعصية”.

Kizuizi cha Tatu : Ni kizuizi cha Maasi.

📕[الجامع للمؤلفات والرسائل (٢٤٦/١٥).

Maelezo ya mfasiri :

Hivi ndivyo vizuizi vinavyomzuia mtu kusimama sawa sawa katika dini iliyonyooka :

1– Kumshirikisha Allah :Kama mtu atakuwa amemshirikisha Allah ushirikina mkubwa basi mtu huyu atakuwa ametoka katika uislamu na akifa katika hali hiyo bila ya kutubu basi makazi yake ni motoni milele, kwa hiyo mtu huyu atakuwa ameshindwa kupita katika njia iliyonyooka hapa duniani kwa maana hakuishi katika uislamu mpaka kufa kwake.

2-Bida’a (uzushi) katika dini : Mtu ambaye alikuwa akifanya mambo ya uzushi katika dini, na kama utakuwa ni uzushi ambao haumtoi mtu katika uislamu basi bila shaka mtu huyu utakuwa ule upitaji wake katika njia hii iliyonyooka si upitaji wa sawa sawa kwa maana huyu ni yule ambaye uislamu wake una madoa madoa kwa sababu ya bidaa alizokuwa nazo ambazo humzuia na kumuelekea Allah kisawasawa, ama akiwa anafanya bidaa zenye kumtoa katika uislamu basi bila shaka huyo atakuwa ni katika washirikina na hukumu yake itakuwa ni sawa na ya huyo tuliyemtaja katika kigawanyo cha kwanza.

3- Maasi (maovu) : Maovu ni kizuizi cha kumuelekea Allah, na muovu hawezi akapita katika njia iliyonyooka sawasawa kwa maana hawezi akawa muumini wa sawasawa kwa sababu maovu humtia uzito mtu katika kutekeleza maamrisho ya Allah.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 18, 1443H ≈ May 19, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *