WAKATI GANI MWANAMKE ANARUHUSIWA KUPUNGUZA HIJABU MBELE YA MTOTO MDOGO WA KIUME ?

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

WAKATI GANI MWANAMKE APUNGUZE HIJABU MBELE YA MTOTO MDOGO WA KIUME ?

🔹السؤال:

متى تغطي المرأة وجهها من الطفل الصغير؟

Swali:

Muda gani mwanamke (anawajibika) kufunika uso wake mbele ya mtoto mdogo ?

🔹الجواب:

Jawabu:

لم يقيد الله -عز وجل- ذلك بسنٍ معين،

وإنما قال:

{أَوِ الطِّفْلِ الَّذِينَ لَمْ يَظْهَرُوا عَلَى عَوْرَاتِ النِّسَاءِ﴾

[النور:٣١]

Allah -aliyeshinda na kutukuka- hakulifunga hilo kwa umri maalumu, na hakika (Allah) amesema:

{au watoto ambao hawajajua mambo yanayohusu uke.

فإذا كان هذا الطفل:
لا يأبه بالمرأة،
ولا يلتفت إليها،
ولا يذكر أوصافها ؛
فإنه لا حرج عليها أن تكشف وجهها عنده،

basi akiwa huyu mtoto :

Hanampango na mwanamke ,
na wala hamgeukii (pindi anapomuona),na wala hataji sifa zake,basi bila shaka hakuna ubaya kwa huyo (mwanamke) kufungua uso wake mbele ya (mtoto) huyo.

أما إذا علم من :
نظراته
وتتبعه النساء أن فيه شهوة؛
فإنه يكون هنا قد اطلع على عورات النساء،
فلا يحل للمرأة أن تكشف أمامه،

ama ikijulikana kuwa ana matamanio ,kwa utezamaji wake,kuwafuatilia kwake wanawake ,basi bila shaka (muda huo) atakuwa anajua mambo yanayohusu uke/tendo la ndoa, basi si halali kwa mwanamke kufungua (uso) mbele yake.

وفي الغالب أن من بلغ عشر سنوات فإنه يطلع على عورات النساء.

na mara nyingi kuwa aliyefika miaka kumi , bila shaka hujua mambo yanayohusu uke .

📔 المصدر:

سلسلة اللقاء الشهري – الشيخ ابن عثيمين رحمه الله – اللقاء الشهري (٣٧)

Maelezo ya mtarjumu:

Hiki ni kipimo cha mwanamke kumjua mtoto mdogo ambaye anaruhusiwa kumpunguzia hijabu mbele yake kama vile kuacha sura wazi ,kwa maana akiwa mtoto ni katika wale ambao si haramu kumuoa huyu mwanamke milele.

Mwanamke ataruhusiwa kupunguza hijabu kwa mtoto ikiwa huyo mtoto hajafikia umri wa matamanio yaani kutamani tendo la ndoa na katika ishara ya hilo la kutofikia hatua ya kujua habari za tendo la ndoa ni kama hizi alizozitaja sheikh -Allah amrahamu-:

1- Kutowajali wanawake yaani hana mpango nao mfano akimuona mwanamke kwake ni kama kamuona mwanamume.

2- Hawatezami wanawake kwa matamanio .

3- Na wala hazungumzi kuhusu sifa za wanawake mazungumzo ambayo ni ishara kuwa anatamani tendo la ndoa.

Kwa hiyo ikiwa hakukudhihiri ishara hizi na nyinginezo kwa mtoto ambazo hujulisha kuwa huyo mtoto ameshaanza kufahamu masuala ya tendo la ndoa basi muda huo mwanamke haruhusiwi kupunguza hijabu mbele yake kama vile kuweka uso wake wazi, na mara nyingi mtoto anapofikia umri wa miaka kumi huanza kuwa na hisia hizi kama alivyosema sheikh .

Mtarjumu:Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy.

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita 15, 1443H ≈ October 21, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *