Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
WANADAMU WANATOFAUTIANA KAMA INAVYOTOFAUTIANA ARDHI.
قال تعالى:
Amesema (Allah) – aliyetukuka:
{ وَلَقَدْ خَلَقْنَا الْإِنْسَانَ مِنْ سُلَالَةٍ مِنْ طِينٍ }
{ Na bila shaka tumemuumba mwanadamu kutokana na udongo uliotolewa kila sehemu }
المؤمنون 12
Al-muuminuun (12)
التفسير النبوي
Tafsir ya Mtume – Swala na Salamu za Allah zimfikie –
عن أبي موسى الأشعري رضي الله عنه عن النبي صلى الله عليه وسلم قال:
Kutoka kwa Abii Musa Al-‘ash’ariy – Allah amridhie – kutoka kwa Mtume – Swala na Salamu za Allah ziwe juu yake – amesema:
إن الله عز وجل خلق آدم من قبضة قبضها من جميع الأرض فجاء بنو آدم على قدر الأرض جاء منهم الأبيض والأحمر والأسود وبين ذلك والخبيث والطيب والسهل والحزن وبين ذلك.
Bila shaka Allah – mwenye nguvu na aliyetukuka – amemuumba Adam kutokana na gao alilolishika kutoka ardhi yote, wakaja wanadamu kwa kadri ya ardhi, Wakaja (wanadamu) miongoni mwao weupe, wekundu na weusi, na baina ya (rangi) hizo na wabaya na wazuri (kitabia) na walaini, na wagumu, na baina ya (tabia) hizo.
أخرجه أحمد والترمذي وصححه الألباني
Maelezo ya mtarjumu:
Kama ilivyokuwa ardhi inasifa fofauti tofauti, kuna ardhi mzuri na mbaya, kuna ardhi laini ambayo ni sifa ya mwanadamu mpole na mwenye tabia nzuri, na kuna ardhi ngumu na hii ni sifa ya mwanadamu mwenye moyo mgumu na ukatili,
Na makusudio ya ardhi mzuri hapa ni muumini yaani muislamu wa sawa sawa ambaye huwa na manufaa matupu, na ardhi ya chumvi makusudio ni kafiri ambaye huwa ana madhara matupu!
Mtarjumu: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Toleo la tatu: Mfungo sita 13, 1443H ≈ October 19, 2021M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•