Wanaume kuhudhuria mashindano ya Qur’ani kwa wanawake!
حُكْمُ إِقَامَةِ مُسَابَقَةِ الْقُرْآنِ الْكَرِيمِ لِلنِّسَاءِ بِحُضُورِ الرِّجَالِ.
Hukumu ya kuweka mashindano ya qurani tukufu kwa wanawake na wakahudhuria wanaume.
ترتيل البنات للقُرْآن بحضرَةِ الرِّجال لا يَجُوزُ، لِما يُخشَى في ذلك من الفِتْنةِ بِهنَّ، وقد جاءت الشريعةُ بسَدِّ الذَّرائعِ المُفْضِيَة للحرَامِ.
Mabinti kusoma qurani katika hadhara ya wanaume haifai, kwa sababu ya kile kinachohofiwa kutokana na hilo ambalo ni kufitinika na hao (mabinti) na bila shaka sheria imekuja kuzuia njia zinazopelekea katika haramu.
[فتاوى اللجنة الدائمة/ج4 – ص 155]
Maelezo: Sheria imeharamisha mambo kadhaa kwa sababu ni njia ya kuingia katika haramu.
mfano: Aliyeingia katika ibada ya hija/umra ni haramu kwake kutumia manukato kwa sababu ni kiitio /kichocheo cha tendo la ndoa. Ni haramu kwa mwanamke kusafiri peke yake bila ya mwanaume ambaye ni haramu kumuoa milele au mumewe kwa sababu kusafiri peke yake ni njia kutendeka machafu. Na mengine mengi ambayo sheria imeyaharamisha kwa sababu ni njia ya kuingia katika haramu na katika hayo ni hili la wanaume kuhudhuria mashindano ya wanawake/wasichana kwa kusikiliza kisomo chao.
Mfasiri: fawaidusalafiya.net
Imeandaliwa: Tarehe 20/ Jumaadal-ulaa, 1442H ≈ 04/ Jan, 2021M. Tembelea website yetu: https://www.fawaidusalafiya.net
#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Kupata faida nyingi jiunge nasi Telegram, bonyeza hapa : ⬇️ https://t.me/fawaidussalafiyatz https://t.me/Darasazandoa •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•