WINGI WA KUMBEBA MTOTO MCHANGA!

قال ابن القيم – رحمه الله:

Amesema Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu:

فصل: كثرة حمل المولود،

Sura (inayozungumzia) : wingi wa kumbeba mtoto mchanga,

وينبغي أن يمنع حملهم،

Na inatakikana kuzuia kuwabeba (watoto wachanga),

والطواف بهم،

Na kuzunguka nao (huku na huku),

حتى يأتي عليهم ثلاثة أشهر فصاعدا،

mpaka wafikiwe na miezi mitatu na kuendelea,

لقرب عهدهم ببطون الأمهات،

Kwa sababu ya ukaribu wao na matumbo ya mama zao,

وضعف أبدانهم.

Na (kwa sababu ya) udhaifu wa miili yao.

📚 تحفة المودود بأحكام المولود لابن قيم الجوزية، دار ابن حزم، بيروت-لبنان، ط ١، ١٤٢٤ ه‍ – ٣..٢ م، ص ١٥١.

Maelezo ya Mfasiri – Allah amuhifadhi

Maelezo haya ameyaeleza Ibn l-Qayyim – Allah amrahamu – katika mlango wa kumi na sita ambao ndani yake una sura kadhaa kabla ya kutaja sura hivi alisema (hivi) :

الباب السادس عشر،

Mlango wa kumi na sita,

في فصول نافعة في تربية الأطفال تحمد عواقبها عند الكبر.

Katika sura zenye manufaa katika kuwalea watoto wadogo (ambazo) matokeo yake ni mazuri (watakapokuwa) wakubwa.

Ufafanuzi:

Kwa hiyo kukithirisha kumbeba beba mtoto mchanga na kuzunguka nae huku na huku kitendo hiki kinamadhara kwake kwa baadae atakapokuwa mkubwa, na kinyume chake kuna faida yaani mtoto mchanga asikithirishwe kubebwa bebwa huku na huku bali alazwe au ashikwe na mama yake pindi anapotaka kumnyonyesha n.k

Ameandaa: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy – Allah amuhifadhi

Dar es salaam, Tanzania
Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz
Jiunge nasi upate faida mbalimbali.

Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi, sambaza kama ulivyopokea bila kubadilisha chochote.

Kupata faida nyingi jiunge na channel yetu ya Telegram kwa kubonyeza kiunganishi hiki: ⇩

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Pia jiunge nasi katika Instagram, Twitter, facebook na you tube:
@fawaidussalafiyatz

   •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *