Wingi wa njia za kulingania

https://www.fawaidusalafiya.net

Amesema Sheikh ibn Uthaimin – Allah amrahamu:

Njia za kulingania ni nyingi:

Kulingania si haswa mtu kusimama na kuzungumza, Kulingania kunakuwa kwa kuzungumza na kunakuwa kwa kuandika na kunakuwa kwa dhati ya kitendo (kinachofanywa). Mwanadamu ambaye unamuamini utajikuta kuwa unaangalia lipi alilolifanya na unafanya mfano wake. Huku ni kulingania, hii ni aina ya ulinganiaji. Bali huwenda kukawa kulingania kwa kutenda na kufanya kuna athari yenye nguvu zaidi kuliko kulingania kwa ulimi.

Kiunganishi cha sauti ya Sheikh: https://youtu.be/lZHM2GUFlEo

Maelezo ya Mfasiri:

Kulingania kwa matendo kuna athari kubwa kuliko kwa maneno kama ilivyotokea katika tukio la sul-hu ya Hudaibiyah, baada ya waislamu kuzuiliwa kuingia Makkah kutekeleza ibada ya umra, Mtume – swala na salamu za Allah – aliwaamrisha waislamu wachinje vichinjwa vyao vya ibada na wanyoe nywele zao au wapunguze, Lakini Maswahaba hawakuchinja na wala hawakunyoa kwa huzuni na mojonzi waliyokuwa nayo ya kuzuiliwa na ibada ya Umrah, mpaka pale Ummu Salamah – Allah amridhie – mke wa Mtume alipomwambia Mtume aanze kuchinja yeye na kunyoa basi Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie- akamtoa ngamia wake akamchinja na akamuita kinyozi akaanza kunyoa hapo ndipo maswahaba wakaanza kuchinja na kunyoa mpaka wakakaribia kukatana, kwa ajili hii ndio maana kunasemwa:

الفعل أبلغ من القول

Kitendo kina athari zaidi kuliko kauli.

Kwa hiyo unaweza ukalingania kwa vitendo vyako mfano unapokuwa katika daladala na konda akakuzidishia chenchi ukamkumbusha na ukampa pesa yake iliyozidi bila shaka utaacha athari kwa konda na watu waliolishuhudia tukio hilo, vile vile mfanya biashara akiuza kwa misingi ya kisheria anaweza akalingania dini ya Allah hapo hapo Sokoni kwake, vile vile daktari wa kiislamu n.k, njia za kulingania ni nyingi mno kama alivyosema Sheikh – Allah amrahamu.

Mzungumzaji: Sheikh Ibn Uthaimin

Mfasiri: fawaidusalafiya.net Imeandaliwa: Tarehe 20 – Safar – 1442H ≈ 07 – October – 2020M.

Kiunganishi: https://t.me/fawaidussalafiyatz Kupata faida nyingi ungana nasi Telegram kwa kubonyeza link hii: https://t.me/fawaidussalafiyatz

Jiunge nasi: Instagram, Twitter, facebook na you tube: @fawaidusalafiyatz

#Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu. •┈┈┈┈••✦✿✦••┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *