wingi wa wanafunzi na uchache wa wanafunzi kwa sheikh !

هذا الإمام الأوزاعي- رحمه الله-يقول:

Huyu imamu Al-auza’iy-Allah amrahamu -anasema :

مات عطاء بن أبي رباح يوم مات، وهو أرضى أهل الأرض عند aالناس،

Alifariki ‘Atwaa bin Rabah siku aliyofariki na hali yeye ni mtu anayeridhiwa zaidi na watu ardhini,

وما كان يشهد مجلسه إلا تسعة أو ثمانية.

(pamoja na hivyo) hakukuwa wanao hudhuria kikao chake (cha kufundisha) isipokuwa (watu) tisa au wanane

[سير أعلام النبلاء (٨٤/٥)

Maelezo ya mfasiri :

Kuhudhuria watu wengi kwa mtu fulani hakujulishi kuwa yeye ni mwanachuoni au manhaji yake imesalimika, na wala kutohudhuria watu wengi hakujulishi kuwa yeye si mwanachuoni au manhaji yake haikusalimika na huyu ‘Atwaa bin Rabah alikuwa ni mwanachuoni mkubwa wa Makkah na Mufti wao, na pindi alipofariki waliulizwa watu wa Makkah :

“Vipi alikuwa ‘Atwaa kwenu? “, wakasema :

مثل العافية ما يعرف قدرها إلا إذا فقدت

“ (Alikuwa) mfano wa afya haijulikani nafasi yake ila pindi itakapokosekana ”

na pia katika hadithi ndefu ya Mtume -swala na salamu zimfikie -aliyokuwa akielezea watu watakaoingia peponi bila ya hesabu wala adhabu, ndani ya hadithi hiyo akaelezea kuwa yeye Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie – alioneshwa nyumati (mataifa) mbalimbali akasema hivi :

.. فَرَأَيْتُ النبيَّ ومعهُ الرُّهَيْطُ، والنبيَّ ومعهُ الرَّجُلُ والرَّجُلانِ، والنبيَّ ليسَ معهُ أحَدٌ،..

Basi nikamuona Nabii akiwa pamoja na watu kuanzia watatu na kuendelea wasiozidi kumi, na Nabii (mwingine) akiwa pamoja na mtu mmoja au wawili ,na Nabii (mwingine) hana mtu yeyote..

رواه البخاري ومسلم.

Faida tunayoipata hapa sisi walinganiaji, au wale masheikh na wanafunzi wenzangu tusiangalie wingi bali tufikishe na tufundishe tukitaraji ujira wetu mbele ya Allah, na wala tusitafute wafuasi katika mitandao mbalimbali ya kijamii kwa kupitia faida mbalimbali tunazozisambaza, na kujiepusha na makusudio hayo ni dalili ya ikhlaswi ni dalili ya kufanya matendo kwa ajili ya Allah, ama kufundisha au kueneza faida kwa kuangalia wingi wa watu bila shaka ni ishara ya kukosa ikhlaswi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo mosi 23, 1443H ≈ May 24, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *