Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
مكروهات الذكاة.
YANAYOCHUKIZA (KATIKA) KUCHINJA 🗡️
قال الشيخ ابن عثيمين – رحمه الله:
Amesema Sheikh ibn ‘Uthaimin – Allah amrahamu-:
للذكاة مكروهات ينبغي اجتنابها فمنها:
Kuchinja kuna mambo yanayochukiza yanayotakikana kuachwa, miongoni mwake (ni):
١ – أن تكون بآلة كآبة أي غير حادة، وقيل يحرم ذلك وهو الصحيح.
٢- أن يحد آل الذكاة، والبهيمة تنظر .
٣-أن يذكى البهيمة والأخرى تنظر إليها
1 – (Uchinjaji) ukawa kwa kifaa butu kwa maana kisichokuwa kikali, na kumesemwa (kuwa) hilo ni haramu na hiyo ndiyo (kauli) sahihi.
2 – (Mchinjaji) akakinoa kifaa cha kuchinjia na hali ya kuwa mnyama anakiona.
3 – Akamchinja mnyama na mwingine anamtizama.
٤ – أن يفعل بعد التذكية مايؤلمها قبل زهوق نفسها.
مثل أن يكسر عنقها أو يسلخها أو يقطع شيئاً من أعضائها قبل أن تموت، وقيل يحرم ذلك وهو الصحيح.
4 – Kufanya lile litakalomuumiza baada ya kumchinja kabla ya kutoka roho.
Mfano akamvunja shingo yake au (akawa) anamchuna au akakata chochote katika viungo kabla ya kufa ,na kumesemwa (kuwa) hilo ni haramu na hiyo ndiyo (kauli) sahihi.
📚 تلخيص أحكام الأضحية والذكاة (٤٧)
Maelezo ya muandaaji:
Haifai kumchinja mnyama kwa kifaa butu, yaani kisichokuwa kikali tena kauli sahihi jambo hili ni haramu, kama alivyosema Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie-:
” .. وَإِذَا ذَبَحْتُمْ فَأَحْسِنُوا الذِّبْحَةَ، وَلْيُحِدَّ أَحَدُكُمْ شَفْرَتَهُ، وَلْيُرِحْ ذَبِيحَتَهُ”.
” Na pindi mnapochinja chinjeni kwa ufanisi (vizuri) na mmoja wenu akinoe kisu chake na akistareheshe kichinjwa chake “.
Ufafanuzi wa hadith:
Kauli yake Mtume – swala na salamu zimfikie- :
“Na akistareheshe kichinjwa chake”
Maana yake: Apitishe kisu kwa haraka na kwa nguvu ili yule mnyama afe mapema atakuwa amempumzisha kutokana na maumivu.
Na vile vile haifai kunoa kifaa cha kuchinjia hali ya kuwa mnyama anaangalia sawa sawa awe mmoja au wengi kama lilivyothibiti katazo hili kutoka kwa Mtume – swala na salamu zimfikie – kutoka kwa ibn ‘Abbas – Allah amridhie-:
مرَّ رسولُ اللهِ صلَّى اللهُ عليْهِ وسلَّمَ على رجُلٍ واضِعٍ رِجْلَه على صَفحةِ شاةٍ وهوَ يُحدُّ شفرتَه, وهيَ تلحَظُ إليه ببصَرِها, قال: أفلا قَبلَ هذا؟ أو تريدُ أن تُمِيتَها مَوتاتٍ؟
(Siku moja) Mtume – swala na salamu za Allah zimfikie – alipita kwa mtu alikuwa ameweka mguu wake katika upande wa shingo ya mbuzi (akijiandaa kumchinja) na hali akikinoa kisu chake na hali ya kuwa huyo (mnyama) akikiangalia hicho (kisu), akasema (Mtume) – swala na salamu za Allah zimfikie- : Si ingekuwa bora ungekinoa kabla ya kuja kumchinja ili asikuone? au unataka kumuua vifo vingi?
📚 صحيح الترغيب, الصفحة أو الرقم: (١٠٩٠)
Ufafanuzi :
Uislamu ni dini ya Allah inayoamrisha kuwafanyia huruma viumbe hata wanyama, unaponoa kisu mbele ya mnyama huku ni kumtia hofu na kumtisha, kisha ukija kumchinja utakuwa kana kwamba umemuua vifo vingi yaani kifo cha kumtisha na kumchinja.
Na vilevile kumchinja mnyama mbele ya wenzake ni kumuadhibu na haifai kufanya hivyo na vile vile kumchuna ngozi au kumkata viungo kabla ya kufa na kukata roho haifai ni katika kumuadhibu.
🗓️ Tarehe: 09 – Dhul-hijjah – 1441H ≈ 30 – July – 2020M.
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Iliandaliwa: 9 -Dhul-hijjah – 1441H ≈ 30- July- 2020M ,ikarushwa tena : 4-Dhul-hijjah-1442H=14-Jul-2021M
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•