Yanayohusiana na funga ya Ramadhani

Makala namba (1)

نزول المذي في رمضان.

☞ Kutokwa na madhii mchana wa Ramadhani

السؤال:

Swali: 📂
يقول:

Anasema (muulizaji):

رجل قبل امرأته في نهار رمضان،

Kuna mtu amembusu mke wake katika mchana wa Ramadhani,

فنزل منه مذي،

Na akatokwa na madhii,

فهل يفسد صومه ؟

Je, funga yake inaharibika ?

الجواب:

Jawabu: 📚

المذي فقط ما يفسد الصوم،

Madhii pekee hayaharibu funga,

على كذا المذي فقط ما يفسد الصوم،

Kutokwa na madhii pekee hakuharibu funga,

وإنما الذي يفسد الصوم نزول المني.

Na hakika si vinginevyo ambalo linaharibu funga ni kutoka manii.

📥 المصدر:

Chanzo: (link ya kupata fatwa ya Sheikh hii hapa): 👇🏽

https://www.alfawzan.af.org.sa/en/node/14891

Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Madhii: Ni maji mepesi yenye kuteleza yanatoka wakati mtu anapobanwa na matamanio na yanapomtoka hajihisi ladha bali humtoka mtu pindi anapohisi matamanio tu ima kwa kubusu au kutizama au kukumbuka na kufikiri hutoka maji haya, na wala si lazima dhakari isimame, na hukumu yake ni najisi anatakiwa aoshe uume wake wote na kokwa zake mbili, na kama yameingia katika nguo basi aoshe sehemu husika ya nguo palipo na madhii au baadhi ya wanavyuoni wanaona kuwa inatosha kunyunyuzia maji ikiwa ni nguo.

Manii: Ni maji meupe mazito humtoka mwanadamu kwa matamanio na hutoka kwa kuchupa na hufuatiwa na kuchoka (kulegea) na huwa na harufu kama la ule weupe wa yai unapokauka, au harufu ya ngano aliyokandwa . na hukumu yake si najisi ila aliyetokwa na manii anawajibika kuoga janaba, na kama mfungaji atambusu mkewe au kumkumbatia na akatokwa na manii basi funga hiyo imeharibika anawajibika kuja kuilipa.

Kwa faida: kuna maji yanayoitwa Wadyu ambayo ni maji meupe mazito hutoka baada ya mkojo na hukumu yake ni hukumu ya mkojo yaani ni najisi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shabani 13, 1443H ≈ Mar 16, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *