Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net
Makala namba (10)
سحب الدم للتحليل.
☞ Kutoa damu kwa ajili ya kupima
السؤال:
Swali: 📂
هل سحب الدم للتحليل يجوز في نهار رمضان ؟
Je, kutoa damu kwa ajili ya kupima kunaruhusiwa katika mchana wa Ramadhani ?
الجواب:
Jawabu: 📚
الدم اليسير لا بأس،
Damu chache hakuna ubaya,
لا بأس في سحب الدم للصائم،
Hakuna ubaya katika kutoa damu kwa mfungaji,
إذا كان قليلا،
itakapokuwa (damu) ni chache,
لا يؤثر هذا.
Hili haliathiri (funga).
📥 المصدر:
Chanzo: (link ya kupata fatwa ya Sheikh hii hapa): 👇🏽
Maelezo ya mfasiri :
Kutoa damu nyingi kwa maana kuchangia damu nyingi mchana wa Ramadhani baadhi ya wanavyuoni wanakufananisha na kupiga chuku ,kama ilivyokuwa kupiga chuku kunaharibu funga katika madhehebu ya imamu Ahmad ,lakini madhehebu ya wanachuoni wengi zaidi yakiwemo ya madhehebu ya kishafii kupiga chuku hakuharibu funga lakini ni bora zaidi mtu asifanye wakati wa funga kwa sababu ya kanuni inayosema :
يستحب الخروج من الخلاف
Inapendeza kutoka katika tofauti (za wanachuoni).
Na hapa kujitoa katika tofauti ya wanachuoni ni kutopiga chuku mchana wa funga, lakini kama atapiga chuku funga yake haijaharibika katika madhehebu yetu na madhehebu ya wanachuoni wengi zaidi kama alivyosema Annawawiy -Allah amrahamu – , ama kutoa au kuchangia damu kama kukiwa kutampelekea katika madhara basi itakuwa ni haramu.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 24, 1443H ≈ Mar 27, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•