Makala namba (11) .
وسائل تعين على الطاعة.
☞ Nyenzo zinazosaidia kumtii (Allah)
السؤال:
Swali: 🎤
ما أهم الوسائل التي تعين المرأة على الطاعات في شهر رمضان ؟
Ni zipi nyenzo muhimu zaidi zinazomsaidia mwanamke juu ya kufanyaa twaa katika mwezi wa Ramadhani ?
الجواب:
Jawabu: 📚
الوسائل التي تعين المسلم رجلاً كان أو امرأة على الطاعات في رمضان هي:
Nyenzo ambazo humsaidia muislamu sawa sawa awe mwanamume au mwanamke juu ya kufanya twaa katika (mwezi wa) Ramadhani ni (hizi) :
١- مَخَافة الله سبحانه وتعالى،
1 – Kumuogopa Allah – utakasifu ni wake na ametukuka,
واعتقاد أنه مطلع على العبد في جميع أفعاله وأقواله ونياته،
Na kuitikadi kuwa yeye (Allah) ni mwenye kumtizama mja katika vitendo vyake vyote na maneno yake na nia yake,
وأنه سيحاسبه على ذلك.
Na kwamba yeye (Allah) atamuhesabu juu ya hayo.
فإذا شعر المسلم بهذا الشعور،
Basi pindi muislamu atakapohisi hisia hii,
اشتغل بالطاعات وترك السيئات،
Atajishughulisha na twaa na kuacha maasi,
وبادر بالتوبة من المعاصي.
Na atafanya haraka kutubu kutokana na maasi (maovu).
٢ – الإكثار من ذكر الله وتلاوة القرآن لأن ذلك يلين القلب،
2 – Kukithirisha kumtaja Allah na kusoma Qur’ani kwa sababu hilo hulainisha moyo,
قال تعالى:
Amesema Allah aliyetukuka:
{ الَّذِينَ آمَنُوا وَتَطْمَئِنُّ قُلُوبُهُم بِذِكْرِ اللهِ أَلاَ بِذِكْرِ اللهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ }
{ Wale ambao walio amini na zikatulizana nyoyo zao kwa kumtaja Allah sikilizeni kwa kumtaja Allah nyoyo hutulizana }
وقال تعالى:
Na amesema (Allah) aliyetukuka:
{ الَّذِينَ إِذَا ذُكِرَ اللهُ وَجِلَتْ قُلُوبُهُمْ }
{ Wale ambao pindi anapotajwa Allah nyoyo zao hupata hofu }
٣ – تجنب الصوارف التي تقسي القلب وتبعده عن الله، و هي جميع المعاصي،
3 – Kujiepusha na vile vinavyomuondoa (mtu katika twaa) ambavyo vinazifanya nyoyo kuwa ngumu na kuziweka mbali na Allah, nayo ni maasi yote,
ومخالطة الأشرار وأكل الحرام،
Na kuchanganyika na waovu na kula haramu,
والغفلة عن ذكر الله عز وجل،
Na kughafilika na kumtaja Allah – aliyeshinda na mwenye nguvu,
ومشاهدة الأفلام الفاسدة،
Na kuangalia filamu mbaya.
٤ – بقاء المرأة في بيتها وعدم خروجها منه إلا لحاجة،
Mwanamke kubakia nyumbani kwake na kutotoka humo (ndani) ila kwa haja,
مع سرعة الرجوع إليه إذا انقضت الحاجة.
Pamoja na kurejea haraka pindi kutakapomalizika (hiyo) haja.
٥ – النوم بالليل لأنه يعين على القيام مبكراً من آخر الليل،
5 – Kulala usiku kwa sababu hilo husaidia kusimama mapema mwishoni mwa usiku,
ويخفف النوم بالنهار حتى يتمكن من أداء الصلوات في مواقيتها، ويستغل وقته بالطاعات.
Na apunguze usingizi mchana ili aweze kutekeleza swala katika nyakati zake, na atumie fursa ya wakati wake kwa twaa (ibada).
٦ – حفظ اللسان من الغيبة والنميمة،
6 – Kuuhifadhi ulimi kutokana na usengenyi na umbea,
وقول الزور، والكلام المحرم، و شغله بالذكر،
Na maneno ya uzushi, na maneno ya haramu, na kuushughulisha (ulimi) kwa kumtaja Allah.
📥 المصدر:
Chanzo: (link ya kupata fatwa ya Sheikh hii hapa): 👇🏽
Maelezo ya mfasiri:
Hizi ni nyenzo na njia zinazompelekea mtu kumcha Allah ndani ya Ramadhani na nje ya Ramadhani ,nyingi katika hizi zinawahusu wote wanawake na wanaume, na nyingine ni haswa kwa wanawake kama vile kutotoka nyumbani ila kwa haja.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 26, 1443H ≈ Mar 29, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•