Yanayohusiana na funga ya Ramadhani

Makala namba (12)

فتاوى النساء في رمضان.

☞ Fatawa za wanawake katika (mwezi wa) Ramadhani,

امرأة يخرج منها دم مصحوب بصفرة في غير عادتها الشهرية،

Mwanamke anatokwa na damu inayoambatana na (rangi ya) unjano njano katika siku zake zisizokuwa za ada ya mwezi (hedhi),

وقد استغرقت معها الشهر كله وصامت في ذلك،

Huenda ikamaliza (hiyo hali) pamoja nae mwezi mzima na (yeye) akafunga katika (hali) hiyo,

فهل يكفي صومها في ذلك أم تقضيه؟

Basi je, yamtosha funga yake katika (hali) hiyo au atazilipa ?

الجواب:

Jawabu: 📚

تقول أم عطية رضي الله عنها:

Anasema mama ‘Atwiyyah – Allah amridhie –

{ كنا لا نعد الصفرة والكدرة شيئاً }

{ Tulikuwa hatuzingatii unjano njano na uchafu (kuwa ni) chochote (katika hedhi) }

هذا رواية البخاري،

Hii ni riwaya ya Al-bukhariy,

ورواية أبي داود:

Na riwaya ya Abii Dawuud:

{ كنا لا نعد الصفرة والكدرة بعد الطهر شيئاً }

{ Tulikuwa hatuzingatii unjano njano na uchafu baada ya kutwaharika (kuwa ni) chochote (katika hedhi) }

وعلى هذا،

Na juu ya hili,

فإذا تطهرت المرأة من الحيض ونزل منها صفرة أو كدرة،

Basi pindi mwanamke atakapojitwaharisha kutokana na hedhi na akatokwa na unjano njano au uchafu,

فإن هذا لا يؤثر على صيامها،

Basi bila shaka hili haliathiri katika funga yake,

ولا يمنعها من صلاتها،

Na wala halimzuii na swala yake,

فتصلي وتصوم ويجامعها زوجها،

Basi (anatakiwa) aswali na afunge na (anaruhusiwa) amuingilie mumewe,

وهي في حكم الطاهرات،

Na huyo (mwanamke) yupo katika hukumu ya (wanawake) waliokuwa twahara,

إلا أنها عند الصلاة لا تتوضأ للصلاة إلا بعد دخول وقتها،

isipokuwa yeye wakati wa swala hatotawaza kwa ajili ya kuswali ila baada ya kuingia muda wake,

إذا دخل وقت الصلاة،

(Anakusudia)pindi kutakapoingia muda wa swala,

فإنها تغسل فرجها وما تلوث من هذا الخارج،

Basi bila shaka huyo (mwanamke) ataosha utupu wake na (sehemu) zilizochafuka na huo (uchafu) kwa nje,

ثم تعصبه بخرقة،

Kisha atapafunga (mahali hapo) kwa kitambaa,

ثم تتوضأ،
kisha atatawaza,

ثم تصلي فروضاً ونوافل كما تريد. 

Kisha ataswali faradhi na sunnah anazozitaka.

📚 مجموع فتاوى ابن عثيمين (19/263)

Maelezo kutoka kwa mfasiri – Allah amuhifadhi

Al-kudra: Ni damu iliyochafuka rangi yake inafanana na maji yaliyooshewa nyama au rangi ya kahawia

Asswufrah: Ni maji maji yanayofanana na usaha wa njano yaani ni usaha ambao juu yake huelea unjano njano,

Hali hii akiiona mwanamke baada ya kutwaharika yaani baada ya kumaliza muda wake wa hedhi na alama ya kutwaharika ni kutokwa na yale maji meupe meupe au kukauka ikawa akiingiza pamba haitoki na uchafu, akishaona hivyo ajue ametwaharika muda huo kile kinachomtoka baada ya hapo hatokizingatia kuwa ni damu ya hedhi.

Ama akiiona hali hiyo yaani uchafu na unjano njano kabla hajatwaharika mfano mwanamke ambaye ada yake ni siku saba katika siku ya tato wakati wa mchana akaona hali hiyo huyu atakuwa bado hajatwaharika kwa sababu yupo ndani ya siku zake.

Ama hii hali aliyoitaja Sheikh – Allah amrahamu – huyu ni mwanamke ambaye ile hali ya uchafu na unjano njano ipo kwake siku zote au muda mrefu huyu hukumu yake ni kama mwenye maradhi ya kikojo kojo au mwenye maradhi ya kutoa ushuzi muda wote hatoruhusiwa kutawadha mpaka ufike muda wa swala na kujihifadhi sehemu inayotoka najisi.

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Shabani 29, 1443H ≈ Apr 1, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *