Makala namba (4)
القراءة أم الحفظ ؟
Kusoma (Qur’ani) au kuhifadhi ?
السؤال:
Swali: 📂
هل الأفضل في شهر رمضان قراءة القرآن، أم القراءة والحفظ،
Je, ni bora zaidi katika mwezi wa Ramadhani kusoma Qur’ani au kusoma na kuhifadhi,
والتأكد مما تم حفظه من القرآن قبل شهر رمضان ؟
Na ili kupata uhakika na kile alichokihifadhi katika Qurani kabla ya mwezi wa Ramadhani ?
الجواب:
Jawabu: 📚
كونه يمر على القرآن كله،
Kuwa kwake anaipita Qur’ani yote (kwa kuisoma),
ويقرأ القرآن كله أفضل
Na (akawa) anaisoma Qur’ani yote (hivi) ni bora zaidi,
من أنه يحفظ بعض آيات ويرددها،
Kuliko akawa anahifadhi baadhi ya aya na kuzirudia rudia (kuzisoma),
ولا يكثر من التلاوة،
Na (akawa) hakithirishi kusoma,
الحفظ يجعل له وقت آخر،
Kuhifadhi atakuwekea wakati mwingine,
ويجعل رمضان لدراسة القرآن من أوله إلى آخره، هذا أفضل.
Na aufanye (mwezi wa) Ramadhani ni kwa ajili ya kuisoma Qur’ani kuanzia mwanzo wake mpaka mwisho wake, hivi ni bora zaidi.
📥 المصدر:
Chanzo: (link ya kupata fatwa ya Sheikh hii hapa): 👇🏽
https://www.alfawzan.af.org.sa/en/node/14891
Maelezo ya mfasiri :
Ramadhani ni mwezi wa Qur’an kuisoma na kusoma tafsiri yake , Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-alikuwa akisomeana Quran na Jibril kila mwezi wa Ramadhani yaani kila mmoja anamsomea mwenzake kama anavyosema ibn Abbas -Allah amridhie -:
..وَكانَ جبريلُ يلقاهُ في كلِّ ليلةٍ من شَهرِ رمضانَ فيدارسُهُ القرآنَ ..
Na alikuwa Jibril akikutana naye (Mtume) kila usiku katika mwezi wa Ramadhani wakisomeana Quran..
البخاري ومسلم .
Na hapa pia tunajifunza pia kusoma Quran wakati wa usiku ni bora zaidi ya mchana kama walivyosema wanavyuoni.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shabani 17, 1443H ≈ Mar 20, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•