Makala namba (5)
حكم قراءة القرآن في المصحف في صلاة التراويح.
☞ Hukumu ya kusoma Qur’ani katika msahafu katika swala ya taraweh
السؤال:
Swali: 📂
هل تصح القراءة من المصحف في صلاة التراويح ؟
Je, inafaa kusoma kutoka msahafuni katika swala ya taraweh ?
الجواب:
Jawabu: 📚
الذي يعجز عن القراءة حفظاً لا بأس أن يقرأه من المصحف في صلاة التراويح،
Yule ambaye anashindwa kusoma kwa kuhifadhi hakuna ubaya kuisoma (Qur’ani) kutoka msahafuni katika swala ya taraweh,
لأنه سيقرأ القرآن كله من أوله إلى آخره،
Kwa sababu yeye (akifanya hivyo) ataisoma Qur’ani yote kuanzia mwanzoni mpaka mwisho,
فإذا لم يكن حافظا للقرآن،
Na kama akiwa si mwenye kuihifadhi Qur’ani,
فإنه يقرأ من المصحف كان بعض السلف يفعل هذا.
Basi bila shaka yeye atasoma kutoka msahafuni kama walivyokuwa baadhi ya (wema) waliopita wakifanya.
📥 المصدر:
Chimbuko: (link ya kupata fatwa ya sheikh hii hapa): 👇🏽
Maelezo ya mfasiri :
Imamu anatakiwa aswalishe kwa kuhifadhi ama akiwa hajahifadhi na yeye akawa ndiye mwenye kuwaswalisha watu basi ataruhusiwa kuswalisha kwa kushika msahafu kama lilivyothibiti hilo kwa wema waliopita kama vile kwa mama Aisha -Allah amridhie – alikuwa akiswalishwa taraweh na Dhakwan -Allah amrahamu-ambaye alikuwa mtumwa wake na alikuwa akimswalisha na hali ameshika msahafu:
فقد كان لعائشة رضي الله عنها غلام يؤمها من المصحف في رمضان .
Bila shaka mama Aisha-Allah amridhie -alikuwa na mtumwa aliyemuacha huru alikuwa akimswalisha kwa kushika msahafu katika (mwezi wa) Ramadhani.
رواه البخاري معلقاً (٢٤٥/١)
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shanan 18, 1443H ≈ Mar 21, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•