YANAYOHUSIANA NA FUNGA YA RAMADHANI (NO. 8)
قضاء رمضان.
☞ Kulipa Ramadhani
السؤال:
Swali: 📂
ما الحكم إذا أفطر المرء لعذر شرعي في رمضان :
Ni ipi hukumu pindi (mtu) atakapofungulia kwa udhuru wa kisheria katika (mwezi wa) Ramadhani:
كسفر بعيد،
Kama vile (kasafiri) safari ya mbali,
وانتهى رمضان وأتى رمضان الذي يليه،
Na ikaisha Ramadhani na ikaja Ramadhani ambayo inayoifuata hiyo (iliyoisha),
ولكن نسي أن يقضي ذلك اليوم ؟
Lakini alisahau kuilipa siku hiyo (afanye nini) ?
الجواب:
Jawabu: 📚
إذا كان ناسيا يقضيه بعد رمضان،
Pindi atakapokuwa ni mwenye kusahau (basi) atazilipa baada ya (kuisha) Ramadhani (mpya),
وليس عليه إلا القضاء،
Na hakuna linalowajibika juu yake ila kulipa tu,
أما إذا كان ذاكرا لصيامه
Ama akiwa ni mwenye kukumbuka funga yake (anayodaiwa),
وتكاسل حتى أتى عليه رمضان الجديد،
Na akajitia uvivu mpaka ikamjia Ramadhani mpya,
يصوم رمضان الجديد،
Atafunga Ramadhani mpya,
ويقضي ما عليه من رمضان الماضي،
Na atalipa yale (madeni) yanayomwajibikia katika Ramadhani iliyopita,
بعد ما ينتهي رمضان الجديد،
Baada ya kumalizika tu Ramadhani mpya,
ويكون عليه كفارة إطعام مسكين عن كل يوم.
Na kutawajibika juu yake kafara ya kulisha masikini kila siku.
📥 المصدر:
Chanzo: (link ya kupata fatwa ya Sheikh hii hapa): 👇🏽
Maelezo:
kiwango cha kulisha masikini ni kama kile cha fidia tu nacho ni kilo moja na nusu takribani kwa maana ikipungua kidogo haidhuru, na atatoa kwa kila siku atakayofunga kwa sababu ya kuzembea kwake na anatakiwa alipe hii funga kwa haraka yaani baada ya sikukuu tu siku ya pili aanze kulipa:
من ترك الواجب عامدا بغير عذر فإن القضاء يكون على الفور
“Mwenye kuacha (jambo) la wajibu kwa kukusudia bila ya udhuru basi bila shaka kulipa (kwake) kunakuwa kwa haraka.
Na hii ndiyo kauli ya wanavyuoni wengi zaidi kwa maana atalipa pamoja na kuwalisha masikini kwa kutoa kibaba na kumpa masikini mmoja kwa kila siku anayolipa.
Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .
Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz
🗓️ Imeandaliwa: Shaban 21, 1443H ≈ Mar 24, 2022M.
Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.
Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz
•┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•