YANAYOTAKIWA KUCHUNGWA KABLA YA KUZUNGUMZA

https://t.me/fawaidussalafiyatz

Website ingia hapa: https://www.fawaidusalafiyatz.net

📍 قال الشيخ/ سليمان الرحيلي- وفقه الله- :

Amesema shekh Sulaymani Arruhayliy Allah amuwafikishe:

إن الإنسان إذا أراد أن يتكلم، فلا بد أن يلحظ ثلاثة أمور:

Hakika mtu atakapotaka kuzungumza basi hakuna budi achunge mambo matatu :

الأمر الأول: أن يكون كلامه حقا في ذاته.

Jambo la kwanza: Yawe maneno yake ni ya haki katika dhati yake.

الأمر الثاني: أن يكون كلامه حقا في قصده.

Jambo la pili: Yawe maneno yake ni ya haki katika makusudio yake.

الأمر الثالث: أن يكون كلامه حقا في أثره، وإلا فإنه يصمت.

Jambo la tatu: yawe maneno yake ni ya haki katika athari yake, na kama hayakuwa (hivyo) basi anyamaze .

📚 ضوابط الربا صـ ٢٦٠

Maelezo ya mpitiaji:

Haya aliyoyazungumza sheikh -Allah amuhifadhi- yakidhibitiwa basi ni sababu kubwa ya kupungua fitna .

1-Usizungumze lolote isipokua hayo maneno yawe ni ya haki na ni ya kweli yasiwe ya uwongo.

2- Pia makusudio ya mazungumzo yawe ni ya haki ,kwa sababu huwenda mtu akazungumza maneno ya haki lakini makusudio yake ni mabaya au kuharibu, mfano kama vile Makhawariji walipomwambia Aliy- Allah amridhie-

“Haikuwa hukumu isipokuwa ya Allah tu” .

Maneno haya ni haki lakini wao makusudio yao ni kumkufurisha Aliy na maswahaba wengine -Allah awaridhie- ,na ndio maana Aliy -Allah amridhie- alipoyasikia maneno haya akasema:

كَلِمَةُ حَقٍّ يُرَادُ بِهَا بَاطِلٌ!

Maneno yaki lakini unakusudiwa upotevu kwa (maneno) hayo .

3- Vile vile maneno anayoyazungumza yanatakiwa yawe na athari na matokeo mazuri ,kwa sababu maneno yanaweza yakawa ya haki na ya kweli , na mzungumzaji akawa ana makusudio mazuri lakini yakawa hayana athari mzuri kama akiyazungumza, basi muda huo anatakiwa ajizuie, bila shaka hii ni nukta muhimu ya kuchunga athari ya kile unachokizungumza kama athari yake ni mbaya basi usizungumze hata kama ni haki na makusudio yako ni mazuri , kama alivyosema ibn Masuud- Allah amridhie-:

ما أنْتَ بمُحَدِّثٍ قَوْمًا حَدِيثًا لا تَبْلُغُهُ عُقُولُهُمْ، إلَّا كانَ لِبَعْضِهِمْ فِتْنَةً.

Hutowazungumzisha watu mazungumzo (ambayo) hayafahamiki akilini mwao, isipokuwa yatakuwa kwa baadhi yao ni fitna

ذكره مسلمٌ في مقدمة صحيحه

Maana ya maneno haya:

Unatakiwa unapowasimulia watu maneno fulani au unapowafundisha basi chunga ufahamu wao kwa maana waambie maneno ambayo wanaweza kuyafahamu na kuyajua,na uchunge hali zao ,na usiwaambie maneno au ukawapa elimu ambayo hawawezi kuifahamu na ikawa ndiyo sababu ya kutokea fitna kama vile watu wakaikataa haki, au ukafahamika vibaya , kwa hiyo hili lakuangalia matokeo na athari ya kile unachokizungumza ni muhimu mno ! , ni wangapi ambao wameleta fitna na mabalaa kwa sababu ya kuzungumza haki ,na makusudio yake ni mazuri lakini akazungumza maneno ambayo hayastahiki kuzungumza muda huo, au sehemu hiyo , na ndiyo maana wanawavyuoni huyanyamazia baadhi ya mambo kwa kuchunga hili.

Mpitiaji: Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo saba 1, 1443H ≈ November 6, 2021M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz
     •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *