ZAWADI KWA MASHAFI WENZANGU!

🔻قال الفقيه الشافعي ظهير الدِّين جعفر التزمنتي – رحمه الله – عن الاحتفال بالمولد النبوي كما في “السيرة الشامية” (١/ ٤٤٢):

Amesema mwanachuoni mkubwa wa fiqih mshafi Dhwahir ddin Jafar Attizmantiy-Allah amrahamu- kuhusu kusherekea mazazi ya Mtume-swala na salamu za Allah zimfikie- kama (ilivyokuja) katika assirati Sshamiyyah (1/442) :

«هذا الفعل لم يَقع في الصَّدر الأول مِن السَّلف الصالح مع تعظيمهم وحبِّهم له ﷺ :

Hili tendo (la kusherekea Maulid) halikutokea katika (kizazi) cha mwanzo cha wema waliopita pamoja na kumtukuza kwao (Mtume) na kumpenda

إعظامًا ومحبة لا يبلغ جميعنا الواحد مِنهم».اهـ

(walimtukuza) utukuzaji ambao na (walimpenda) mapenzi ambayo sisi wote hatuwezi kumfikia mmoja wao katika wao .

السيرة الشامية ( ٤٤٢/١)

Maelezo ya mfasiri:

Huyu ni katika wanavyuoni wakubwa tena Mshafi mwenzetu anaeleza uzushi wa kusherekea kuzaliwa kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-kwa kutumia kanuni ya kutofanywa na wema waliopita na wa mwanzo wao ni Maswahaba -Allah awaridhie – Maswahaba ambao walikuwa wakimtukuza Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie- na wakimpenda mapenzi ambayo hata kama sisi sote mapenzi yetu tutayakusanya basi hayatoweza kuyafikia mapenzi ya mmoja wao kwa Mtume -swala na salamu za Allah zimfikie-,kwa hiyo jambo lolote katika dini ambalo hawakulifanya Maswahaba basi hilo jambo ni uzushi kama alivyolisema hilo pia mwanachuoni wetu wa kishafi Ibn Kathir katika tafsiri yake ya suratul-ahqaaf aya ya 11:

وَقَالَ الَّذِينَ كَفَرُوا لِلَّذِينَ آمَنُوا لَوْ كَانَ خَيْرًا مَّا سَبَقُونَا إِلَيْهِ ۚ

Na waliokufuru waliwaambia Walioamini: “Lau lingalikuwa (hilo la kuamini yale aliyokuja nayo Muhammad) ni la Kheri wasingetutangulia  hao (wanyonge) “

الأحقاف ١١

Akasema ibn Kathiri ambaye ni Mshafi  katika kutafsiri kipande hiki cha aya,  maneno yafuatayo: 

وأما أهل السنة والجماعة فيقولون في كل فعل وقول لم يثبت عن الصحابة : هو بدعة ;

Na ama Ahlusunnah wal-jamaa husema katika kila kitendo na kauli isiyothibiti kutoka kwa Maswahaba hiyo ni bidaa (uzushi)

لأنه لو كان خيرا لسبقونا إليه ؛ لأنهم لم يتركوا خصلة من خصال الخير إلا وقد بادروا إليها

Kwa sababu (Jambo) hilo lau lingekuwa ni la kheri wangetutangulia katika hilo kwa sababu wao hawakuacha jambo lolote katika mambo ya kheri ila bila shaka wameliharakia (kulifanya).

Marejeo:

تفسير القرآن العظيم ،للحافظ أبي الفداء إسماعيل بن عمر بن كثير القرشي الدمشقي الشافعي

Ufafanuzi:

Maneno haya ya ibn Kathir ambaye ni Mshafi mwenzetu yanaonesha wazi kuwa yeyeyote mwenye kulifanya jambo ambalo maswahaba hawakulifanya na akaliegemeza katika dini basi jambo hilo litakuwa ni bidaa (uzushi) na hivi ndiyo wanavyosema Ahlusunnah waljamah, na kwa maneno haya nadhani hukumu ya kusherekea Maulidi itakuwa imefahamika kwa sababu ni jambo ambalo Maswahaba hawakulifanya !

Mfasiri : Abuu Thurayyaa Ismail Seiph Mbonde Asshafiy .

Muandaaji: fawaidusalafiyatz.net
Tembelea website yetu: ☟
https://www.fawaidusalafiyatz.net
Telegram bonyeza hapa: ☟
https://t.me/fawaidussalafiyatz

🗓️ Imeandaliwa: Mfungo sita  12, 1444H ≈ October  8, 2022M.

Muhimu: Vuna thawabu kwa kusambaza faida hizi. Sambaza kama ilivyo, si ruhusa kubadilisha chochote. Tuwe waadilifu.

Jiunge na chennel yetu ya telegram upate faida nyingi, kujiunga bonyeza link hii: 👇🏾
https://t.me/fawaidussalafiyatz

https://t.me/fawaidussalafiyatz

         •┈┈┈┈•✿❁✿•┈┈┈┈•

Comments

No comments yet. Why don’t you start the discussion?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *